29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kizungumkuti kesi ya Mfanyabiashara aliyetapeliwa mamilioni Shinyanga

Na Zephania Kapaya, Shinyanga

JESHI la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limelalamikiwa na Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Rehema Mwagao kwa kitendo cha kumuachia muharifu kinyemela aliyetuhumiwa kutapeli fedha kiasi cha Dola 25,847.50 zaidi ya Sh milioni 48.6.

Akiongea na Waandishi wa Habari hivi karibuni nyumbani kwake mjini Kahama Rehema amesema kuwa mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fabiani Mazali mkazi wa jijini Dar es Salaamu mmiliki wa kampuni ya Natwest Financial Corsultants Ltd inayojihusisha na mikopo ya bank ya kiislamu toka nchini Uingereza.

Amesema Fabiani alikamatwa na polisi Mei, mwaka huu kituo cha polisi Kahama kwa RB KAH/IR/1725/2021 kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kisha kuachiwa kwa dhamana na watu nisio wafahamu lakini mpaka leo nazungushwa bila majibu ya kuridhisha .

Aidha,Rehema amesema kuwa makubaliano yao yalikuwa ni kupatiwa mkopo wa mashine kutoka kampuni ya OCEAN EXTRUSIONS PVT.LTD ya nchini India ambayo ataniunganisha nayo ili nipate mkopo wa mashine kwa riba nafuu ya asilimia tano na kwa malipo ambayo yameandikwa hapo awali.

“Mimi baada ya makubaliano hayo nilimuingizia kiasi cha Dola 25,847.50 sawa na Sh milioni 48.64 kwa thamani ya wakati huo ambao ni mwaka 2016/17 kwenye akaunt namba 0150201257000 katika bank ya CRDB  kwa awamu mbili tofauti,” amesema Rehema.

Aidha, Rehema amesema ameshangazwa na alishangazwa na kauli ya polisi kuwa kesi hiyo imegeuzwa kutoka jinai na kuwa madai ambapo amesema hajawahi kukubaliana nae toka akamatwe na wala hatujawahi kukutana nae sehemu yoyote.

Kwa upande wake mtuhumiwa ambaye ni Fabiana Mazari, alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi alikiri kufanya nae biashara na kwamba yeye siyo tapeli huku akisisitiza kuwa anachojua kuwa biashara hiyo ni halali na alimpa mkataba halali na kwamba yeye ndiye aliyevunja mkata bila kufuata sheria.

“Mkataba ni siri ya ofisi siwezi kuuzungumza, hivyo hayo niliyo yazungumza yanatosha ninacho omba afuate utaratibu aache kutisha napia mchunguze habari hizi ili muweze kutenda haki sehemu zote mbili,” amesema Fabiana.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, George Kyando amelithibitisha kufahamu jambo hilo na kwamba mama huyo alifikisha malalamiko yake ofisini kwake na kwmaba baadaye lilipoona kuna utata waliomba msaada wa kisheria kwenye ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Kahama na kuongeza kuwa walijibiwa kuwa hiyo ni kesi ya madai.

Kwa upande wa Mwendesha Mashitaka wa Mkoa wa Shinyanga, Magreth Ndaweka alisema faili hilo halijui na halijafika ofisini kwake hivyo hawezi kusema chochote kuhusu hilo.

“Ninachoweza kushauri aulizwe Mwendesha Mashitaka wa Wilaya ya Kahama nako tuna ofisi huenda yeye akawa ana majibu,” alisema Magreth.

Alipotafutwa Mwendesha Mashitaka huyo wa Kahama aliyejitambulisha kwa jina la Mercy Ngowi alikiri kuelewa shauri hilo huku akisisitiza kuwa mtu pekee anayeweza kulitolea taarifa ni DPP.

Upande wa Ofisi ya DPP Makao Makuu Dodoma kupitia Afisa Uhusiano wake aliyefahamika kwa jina moja la Rebeca alisema kuwa swala hilo liko chini ya mwendesha mashitaka Mkoa na kwamba huyo ndiye anaweza kulijua zaidi.

Mwandishi alilaazimika kumtafuta Mwendesha Mashitaka wa Mkoa wa Shinyanga, Magreth Ndaweka, ambapo alisema kuwa mpaka apate kibali toka kwa DPP kwani maelekezo yalikwisha tolewa kutozungumza chochote na vyombo vya habari kwa mambo ya kiofisi isipokuwa DPP tu na hata hivyo hawezi kusema kitu mpaka faili alione.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles