25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Msoma Vijijini wamshukuru Rais Samia

Na Shomari Binda, Musoma

Wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Wakizungumza leo Jumanne Oktoba 26, kwenye mradi wa barabara mpya ya Mkirira-Kwangwa iliyofunguliwa hivi karibuni, wamesema imekuwa ni msaada mkubwa kupatikana kwa barabara hiyo.

Wananchi hao wa Kijiji cha Mkirira wamedai kuwa kipindi cha nyuma walilazimika kusafiri umbali ea kilometa 15 kwenda hospital ya rufaa ya Mwalimu Nyerere lakini sasa wanasafiri kwa kilometa 4.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la, Mukama Magoti,amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia imekuwa na huruma kwa wananchi kwa kuwajali katika masuala mbalimbalu.

Mukama amesema licha ya barabara hiyo kuwawezesha kufika kwa haraka hospitalini lakini pia inawasaidia katika shughuli za kiuchumi.

“Tunashukuru Rais Samia kwa kuwezesha fedha na kufunguliwa kwa barabara hii na leo imetupa unafuu tofauti na miaka ya nyuma.

“Zipo barabara nyingine katika jimbo letu zilukuea hazipitiki lakini sasa nyingi zinapitika na tunamshukuru pia mbunge wetu, Profesa Sospeter Muhongo kwa ufatiliaji,” amesema Mukama.

Meneja wa Tarura wilaya ya Musoma, Hussein Abbas, amesema serikali imetoa fedha zaidi ya Sh bilioni 1 kwenye halmashauri hiyo na kazi inaendelea kwenye maeneo mbalimbalii.

Upande wake Profesa uhongo, amesema kila eneo la jimbo kumekuwa na kasi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na kuishukuru serikali ya Rais Samia kwa fedha walizopata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles