28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya dini yashauri Seriikali kuharakisha bima ya afya kwa wote

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Kamati ya dini mbalimbali pamoja na wadau wa afya wameishauri Serikali kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote kwani itakuwa mwarobaini wa kusaidia wananchi kupata huduma za afya kwa uhakika.

Hayo yameelezwa Jumatatu Oktoba 25, jijini Dodoma na viongozi mbalimbali wa dini wakati wakichangia katika mkutano ulioandaliwa na Kamati ya dini mbalimbali  uliowakutanisha viongozi wa dini na wadau wa masuala ya afya.

Viongozi hao wa kamati ya dini mbalimbali wamesema kupitisha kwa sheria hiyo kutakuwa mkombozi kwa watanzania ambao wanakosa huduma za afya kutokana na kukosa fedha na wale wenye uchumi mdogo.

Akichangia katika mjadala huo, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Kanisa la Menonite, Nelson Kisare amesema Utafiti ulifanyika walipata  majibu na walitengeneza  kitabu na wnatumia  tafiti kushawishi serikali kuwa na sheria bora ambayo itakuwa inatoa haki kwa kila mwenye uhitaji

“Tumekuwa tukikutana mara kwa mara na kushauriana na leo tumekutana kuendeleza yale mazuri ni kitu gani kifanyike ili iwe ni kitu ambacho ni cha manufaa nipende kutoa shukrani kwa Serikali tumesikia katika hotuba za rais akizungumzia Wizara ya fedha na Mipango  ilete fedha ili muswada huo uweze kupitishwa.Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa juhudi hizi wanazofanya,”amesema.

Mwenyekiti huyo amesema lengo la mkutano ni nini kifanyike ili waweze kupata sheria ambayo itasaidia watu wenye kipato cha chini.

“Sasa tumekutana nini kifanyike ili tuwe na nia moja lengo moja tupime kwa pampja ili tupate sheria ambayo itatusaidia matumaini yetu ni kwamba tutajaliada kwa amani na upendo,”amesema.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Khamis Mataka amesema katika jamii kwa sasa hali ni mbaya hivyo inahitajika sheria ya bima kwa afya iweze kupita ili kuwakomboa watanzania wengi.

“Hali ya jamii ni mbaya tufanye mambo hii sheria iweze kupita ili ituletee nafuu watu wetu na sisi wenyewe,”amesema Mataka.

Kwa upande wake,Mratibu wa Kamati ya amani Taifa,Edmund Matotay amesema wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 vyama mbalimbali viliinadi sera ya bima ya afya kwa wote ambapo vilidai vikichukua Nchi bima ya afya kwa wote itaanza kutumika.

Amesema baada ya uchaguzi Rais( Hayati Dk.John Magufuli) alitamka Serikali ilete mchakato wa muswada wa bima ya afya kwa wote.

“Baadae tuliona Rais pale Ikulu akitamka Serikali ilete bima ya afya kwa wote sisi kama viongozi wa dini tulifurahi sana kwamba Rais ametamka jambo hilo,na katika hotuba Waziri wa Fedha na Mipango na wa Afya waliweka vifungu mbalimbali vya kulipia kaya masikini katika sheria ya bima ya afya kwa wote,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles