26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi mpakani waaswa kuimarisha Uhusiano

Na Denis Sinkonde, Songwe

Wananchi waishio mpakani mwa Tanzania wilayani Ileje mkoani Songwe na Malawi Wilaya ya Chitipa wameaswa kuimarisha uhusiano ili kufungua fursa za kiuchumi kwa mataifa hayo mawili.

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Benedicto Mashiba ametoa ushauri huo Februari 27, 2022 baada ya kutembelea mpaka wa Tanzania katika mji mdogo wa Isongole wilayani Ilejemkoani Songwe na kupokea taarifa ya hali ya mpaka kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Ileje, Anna Gidarya.

Mashiba amesema katika kuhakikisha mpaka huo unafungua fursa za kiuchumi na kibiashara Serikali ya Malawi ina mpango wa kujenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita zaidi ya 30 kutoka Chitipa mpaka daraja la mto Songwe.

Barabara hiyo ni sehemu ya mpaka wa nchi hizo mbili ili kuondoa adha ya usafiri kwa upande wa Chitipa ambapo serikali ya Tanzania imefanikisha kutengeneza barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 50 kutoka mpakani hapo hadi Mpemba na kurahisisha kusafirisha mizigo.

“Wafanyabiashara wa Malawi hupata shida kusafirisha mizigo yao kutoka Tanzania pindi wanapotoka kujumuwa mizigo Tanzania katika boda ya Tunduma na Isongole, hivyo nitaishauri serikali ya Malawi kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo,” amesema Mashimba.

Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya amesema serikali ipo katika mpango wa kujenga kituo cha ushuru wa forodha katika mji wa Isongole.

“Katika kukuza uchumi kwa wananchi serikali ipo katika mpango wa kujenga kituo cha ushuru wa forodha katika mji wa Isongole ili kukuza fursa za biashara za mpakani sambamba na kuongeza mzunguko wa fedha kama ilivyo boda zingine Tanzania kama vile Boda ya Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe na boda ya Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya,” amesema Gidarya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles