32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Monduli wafunguka

?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????NA ELIYA MBONEA, MONDULI
BAADHI ya wananchi wa Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, wamezungumzia hatua ya Mbunge wao, Edward Lowassa, kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania nafasi ya urais, wakisema kuwa anatosha.
Kwa nyakati tofauti, wananchi hao wameliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa wapo nyuma ya kiongozi huyo na wataendelea kumuombea kwa Mungu ili achaguliwe na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
Mkazi wa Dukabovu aliyejitambulisha kwa jina la Thobias Sakaya (43), alisema wao kama wapiga kura wa Monduli wanamkubali kiongozi huyo, kwani ni mchapa kazi na mtu anayefuatilia ahadi zake tofauti na viongozi wengine.

“Sisi tunamkubali, kwani ana uwezo mkubwa wa kuliondoa taifa kutoka hapa lilipo kwenda hatua nyingine zaidi ya maendeleo. Tunamuomba ajiandae na ahamasishe watu kujiandikisha ili wampigie kura.

Mkazi mwingine wa Meserani, Loishiye Kivuyo (28), alisema yeye pamoja na wakazi wenzake watakwenda uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuungana naye katika ‘Safari ya Matumaini’.

“Tunaendelea kumuombea Mungu atampa kusudi la moyo wake na kwa ushirikiano wetu tunaahidi hatutamuangusha,” alisema Kivuyo.

Mkazi mwingine wa Monduli, Samweli Mollel (27), aliiomba CCM ipitishe jina la Lowassa kugombea urais, akisema kuwa ni kiongozi makini na muwajibikaji. Lakini pia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wa Monduli wanapata maendeleo.
“Lowassa hataki mchezo na ni mkali kwenye maendeleo, hilo watu wanalijua na ndiyo maana sisi wananchi wa chini tunaomba achaguliwe kuwa kiongozi wetu,” alisema Mollel.

Mkazi wa Dukabovu, Israel Pallangyo (25) alimuomba Lowassa, endapo akichaguliwa atimize ahadi yake ya ajira kwa vijana, kwani yeye pia ni miongoni mwa vijana walioathirika na ukosefu wa ajira.
“Tunatambua uwezo na nguvu za Lowassa, ni mbunge wetu, tumeona mambo mengi aliyoyafanya hapa jimboni, namuomba akichaguliwa aangalie kwa umakini suala hili la ajira kwa vijana, kama ambavyo mwenyewe amekuwa akisema ni bomu linalosubiri kulipuka,” alisema.

Kwa upande wake, Lazaro Mollel (45), alisema anamuunga mkono Lowassa kwa asilimia 100 na anamuahidi kumsindikiza leo kwenye hatua ya kuanza “Safari ya Matumaini.”

“Tutaendelea kuwa naye hadi siku ya kuanza kampeni, kupiga kura, kwani tuna imani naye katika utendaji,” alisema Mollel.
Klembu Ronda (37), ambaye ni mkazi wa Meserani, alisema ni maombi yake kwa Mungu ili Safari ya Matumani ya Mbunge wake, Lowassa ifanikiwe.
“Namuomba Mungu sana amuongoze. Na akichaguliwa namuomba aboreshe maisha ya Watanzania na hasa ajira kwa vijana,” anasema Ronda.
Naye mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Happiness Yussuf (37), anayeishi Meserani, wilayani Monduli, alisema anamuomba Mungu ili Lowassa apite ndani ya uchaguzi wa CCM, kisha achaguliwe na Watanzania wote kuwa Rais wa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles