23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Kilombero walilia umeme

Na Mwandishi Wetu, Kilombero
WANANCHI wa Kijiji cha Mpanga wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamelalamikia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushindwa kufikisha umeme katika shule ya Sekondari ya Mtenga kijijini hapo.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, wananchi hao walisema hawaelewi kwa nini shule hiyo imeondolewa katika orodha ya shule zinazotarajia kupata umeme licha ya umuhimu uliopo hususan suala la matumizi ya maabara.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao, mkazi wa kijiji hicho, Betram Mhenga alisema vijiji ambavyo vinapaswa kupata umeme kama walivykubaliana awali ni Utengule, Ngalimila na Mpanga ambacho kipo karibu na shule hiyo.
“Kwa kweli sisi wana Mpanga tunashindwa kuelewa ni kwa nini shule hii inakosa umeme na kila siku gari la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linapita likiwa limebeba nguzo kupeleka maeneo mengine na kuacha shule hii ikiendelea kuwa gizani licha ya umuhimu uliopo.
“Kwa nini Mpanga tanaambiwa nguzo zimekwisha wakati tunaona gari la Tanesco linapitisha nguzo kupeleka Utengule?” alihoji Mhenga.
Mhenga alisema taarifa zilizopo ni kwamba Kijiji cha Ngalimila kilichangishwa Sh 100,000 ili ziongezwe nguzo zaidi ya zile walizopangiwa huku mradi ukiwa haujakamilika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpanga, Samweli Kamwelanga alisema anashangazwa na mradi huo kutokuweka kipaumbele kwa huduma za jamii kama shule na vituo vya afya kurahisisha utendaji.
Meneja Tanesco Wilaya ya Kilombero hakupatikana kuzungumzia malalamiko hayo baada ya simu yake kutopatikana jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles