28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Kagongwa, Isaka kuanza kupata maji

Rais Dk. John Magufuli jana Januari 29, amezindua Mradi wa Maji wa Kagongwa na Isaka, Kahama Mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka, Kahama mkoani Shinyanga.

Aidha, katika uzinduzinhuo, Rais Dk. Magufuli alitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Awesu, kuhakikisha kuwa anasimamia kikamilifu miradi mbalimbali ya maji ikiwamo kuwachukulia hatua wakandarasi wazembe

“Mhe Waziri wa Maji na timu yako mmeanza vizuri. Msiwaonee haya Wakandarasi wasiotekeleza miradi kwa wakati. Wananchi wanataka Maji.

“Kuanzia kesho maji yasambazwe katika vijiji vyote hapa, kwa kua maji haya ni ukombozi kwa kinamama waliokua wakitaabika kwa adha ya maji kwa muda mrefu,” amesema Dk. Magufuli.

Mradi huo unahusisha matenki matano yenye uwezo wa lita milioni 2.5, pia urefu wa mabomba ni jumla ya Km 198. Mradi huo una uwezo wa kuhudumia wakazi 115,600 ambapo mijininayotarajiwa kunufaika ni Kagongwa na Isaka na vijijii nufaika ni 22.
Gharama ya mradi ni Sh bilioni 23.1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles