27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi wa Maji Burumawe, kuleta neema kwa wakazi wa Mabwepande

Na Fredrick Msiru -DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam {DAWASA} kupitia Mkoa wa kihuduma Mabwepande imejidhatiti kuwafikishia huduma ya maji wananchi wake kwa kuboresha huduma na kumaliza kwa haraka mradi mdogo wa Maji wa Burumawe unaotekelezwa na Mkoa wa kihuduma DAWASA Mabwepande.

Akiongea kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi wa DAWASA Mabwepande ambaye pia ni Msimamizi wa Mradi huo, Juma Kalemera ameeleza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mapema mwezi Januari 2021 na unatarajia kukamilika mapema mwezi Februari 2021.

Ameongeza kuwa mradi huo umehusisha shughuli ulazaji wa bomba ukubwa wa inchi 3 kwa umbali wa mita 250 na bomba za inchi 2 kwa umbali wa mita 450 na uliogharimu kiasi cha Shiling Milion nne.

“Mradi huu wa Maji Burumawe utanufaisha wakazi wa Burumawe katika mitaa ya Gosheni na Maweni kukamilika kwa mradi huu kutaenda kuwanufaisha kaya zaidi ya 100 kwa kuwapatia huduma ya maji”alifafanua Mhandisi Kalemera,” amesema.

Kwa upande wa Mamlaka, mradi huu utakua na faida kubwa kwani unaenda kuongeza eneo la kihuduma kwa kufikishia wateja wapya huduma ya maji, kitendo ambacho kitaongeza makusanyo na kuipa faida mamlaka”.amesema Mhandisi kalemera.

Wananchi wa Burumawe akiwemo John Minja nao wameonyesha furaha yao baada ya kupelekewa mradi huo

“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar-es-salaam {DAWASA} kwakuweza kutusogezea huduma ya maji katika mitaa yetu ya Gosheni na Maweni, sasa tunaiona neema mbele yetu kwani shughuli zetu nyingi zitakwenda kufanyika kwa wakati na adha ya maji itaondoka katika eneo hili” amesema Minja.

Utekelezaji wa mradi wa Maji Burumawe ni moja ya jitihada zinazoendelea kufanywa na DAWASA katika kuhakikisha dhamira yake ya kuwafikia wananchi wote inatimia ili kuendana na kauli mbiu yake ya kuelekea 2025, kuwafikia wananchi wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles