-Sudan
Wanajeshi wa jeshi la Sudan wamekamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya waandamanaji wawili katika mji mkuu Khartoum, wiki iliyopita.
Mkuu wa baraza la mpito nchini humo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ameamuru uchunguzi kuhusu mauaji ya siku ya Jumanne yaliyotokea nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum.
Pia raia nchini Sudan wameendelea kudai haki kwa serikali ya nchi hiyo kwa vitendo vya ukatili mkubwa ambao umetokea takribani miaka miwili iliyopita.