33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘WANAJESHI’ WAAPA KUIMALIZA SIMBA UFUNGUZI VPL

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Abdulmutik Hadji, amesema kikosi chake kimeiva tayari kuivaa Simba katika pambano la ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara litakalopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Hadji alisema michezo yao ya kirafiki imewajenga kiasi cha kutosha na sasa wanahamishia makali yao kwenye ligi.

“Nafahamu mchezo utakuwa mgumu ukizingatia ni wa ufunguzi wa ligi, lakini kila timu imejiandaa vya kutosha, hakuna  inayohitaji kuanza vibaya na kupata  matokeo yasiyoridhisha, hivyo lazima tupambane na kutimiza malengo ambayo tumejiwekea,” alisema.

Alisema anafahamu Simba imefanya usajili mzuri, lakini na wao wamefanya usajili ikiwa ni pamoja na kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hadji alisema licha ya kwamba kikosi chake kitawakosa baadhi ya nyota wake kama Fully Maganga, Shalla Juma, lakini amewaandaa wachezaji wengine ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

“Tulicheza na Yanga mechi ya kirafiki na kufanikiwa kuwafunga bao 1-0, leo (jana) tumetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda, naamini tuna fursa pia ya kuwaonyesha Simba kwamba tuko imara kwa kuwafunga,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles