25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaharakati watakiwa kuelimisha kuhusu  kumlinda mtoto wa kiume

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Phumzile Mlambo Ngcuka, amewaelekeza  wanaharakati wa kifeminia nchini   kujikita katika kuelimisha kuhusu ulinzi wa mtoto wa kiume kwa mustakabali wa haki  na usawa  wa jinsia.

Phumzile ameyabaisha hayo leo Novemba 7, 2023 jijini Dar es Salaam katika tamasha la jinsia la 15 pamoja na kuadhimisha  miaka 30 Kifeminia la Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP).

Amesema katika harakati za kukataa ukandamizaji wa aina yoyote, pia suala la ulinzi wa mtoto wa kiume linatakiwa kuzingatiwa katika kuendeleza ajenda za kumkomboa.

Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa Jinsia (TNGP), Lilian Liundi.

Amesema ipo haja ya kuwa na majukwaa ya wanaume nchini yenye kueleza yanayowahusu, pia yatumike kuchukua hatua za kupinga ukatili wa kijinsia, ubaguzi dhidi ya wanawake na  wanaokataa ndoa za utotoni

“Wanaharakati wa haki za binaadamu wasiruhusu aina yoyote ya ukatili  kuanzia kuukataa  mfumo dume katika ngazi ya familia na kuongeza kuwa ipo haja ya kuwepo mabadiliko ya kisera na sheria lakini pia jamii kubadilika,” amesema Phumzile.

Amesema  mfumo dume sio rafiki kwa wanawake na hata wanaume  na  umekuwa  ukiendeleza  ubaguzi hivyo ni muhimu kwa wanaume na watoto wakiume miongoni mwa harakati za kupinga  kwani  hii ni karne ya wanaume wenye mshikamano na wenza wao.

Baadhi ya watu waliojitokeza katika tamasha hilo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gema Akilimali, amesema licha ya mtandao huo  kuadhimisha miaka 15 ya usawa wa kijinsia lakini  changamoto bado ni nyingi, kwa  sasa wanahitaji zaidi ushirikiano na Serikali.

Gema amesema katika tamasha hilo la siku nne watatoka na maazimio ya jumla kwani upo mchango wa TGNP katika harakati mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP,  Lilian Liundi amasema tamasha la jinsia  ni jukwaa la kuleta sauti kwa pamoja lenye kujadili na kupanga  mikakati.

“Tamasha hili ni la 15 tangu kuanzishwa  limeweza kuwa na washiriki 2000 hadi 5000 kwa tamasha moja limewafikia watu zaidi ya 35000,”amesema Liliani.

Amesema tamasha hilo limewaleta watu wa ukanda wa Afrika kwa  kwa pamoja na wameendelea kusimama kwenye misingi ya waasisi wao.

Aidha amesema TGNP imejengwa katika  misingi imara  ya haki na kuondoa mifumo kandamizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles