Florence Sanawa
Wanafunzi zaidi ya 873 wa shule ya msingi Tandika Manispaa ya Mtwara mikindani, wako katika mazingira hatarishi baada ya shimo la maji taka kubomoka hivyo kupelekea choo hicho kufungwa na kufanya wanafunzi wa shule hiyo kutumia choo cha shule ya jirani.
Akizungumza na Mtanzania digital, mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Ziada Myao, amesema kuwa shule hiyo ilikuwa na choo ambacho kilikuwa na shimo la maji taka nyuma lakini lilibomoka hali ambayo imepelekea choo hicho kufungwa.
“Shule yetu haina choo sio kwa walimu wala wanafunzi tumekuwa tukitumia choo cha shule jirani hali ni mbaya awali chooo kilichotumika kilikuwa na matundu 14 lakini kimefungwa ujio wa hii kampeni ya shule ni choo,” amesema.