25.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 31, 2023

Contact us: [email protected]

Salam avunja ukimya Harmonize kuondoka WCB

Anna Potinus, Dar es Salaam

Meneja wa msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz, Salam SK amevunja ukimya juu ya taarifa zinazosambaa mtandaoni kuhusu kuondoka kwa msanii Rajab Kahali ‘Harmonize’ katika lebo ya Wasafi (WCB).

Akizungumza na moja ya vyombo vya habari nchini, Salam amesema Harmonize ameshawasilisha barua za kutaka kusitisha mkataba na kampuni ya Wasafi na kwamba wanasubiri taratibu za kisheria ziweze kufuatwa kasha watatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo.

“Harmonize kwa sasa moyo wake hauko WCB lakini kimakaratasi bado hupo kwasababu ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba wake na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kuweza kuvunja mkataba na sisi tumependezwa na kitendo hicho kuona mtu ambaye amesimama na anafuata sheria, inawezekana ameona umefikia wakati kwa yeye kujiendeleza labda kuna vitu ambavyo vilikuwa vinambana anaona akifanya peke yake vinaweza kumfikisha mbele,” amesema.

“Sisi kama Taasisi ya Wasafi tuko radhi kwa yoyote ambaye ataamua kuvunja mkataba na akifuata sheria zote ana Baraka zote kutoka kwetu na chochote anachotaka kushirikiana na sisi muda wowote tuko tayari kwani unapoondoka katika mazingira mazuri inasadia kuacha mahusiano yabaki pale pale,” amesema.

Amesema baada ya kumaliza mazungumzo ya kisheria na Haromize watautangazia umma kwamba ameshaondoka lakini wanaamini kwa sasa ndani ya nafsi yake ameshatoka WCB kwani hayuko radhi kufanya nao kazi tena.

“Hauwezi kumlazimisha mtu kufanya nae kazi kama hayuko tayari, mkataba hata kama una miaka 10 unaweza ukavunja muda wowote unaotaka na tuna uhakika mkataba wake utavunjwa kwa haki na hatodhulumiwa kabisa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,315FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles