25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WATAKA MFUMO WA ELIMU NCHINI UFUMULIWE

ndalichako

Na FERDNANDA  MBAMILA, DAR  ES  SALAAM

MTANDAO wa wanafunzi  Tanzania  (TSNP) umeitaka seriali kuufumua  mfumo wa elimu nchini kwa vile umeghubikwa na mikakati hafifu  katika harakati za kuikomboa elimu ya Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa  Dar es Salaam jana na Umoja huo kwa   shule za sekondari.

Walisema  licha ya  jitihada nzuri za kuinua elimu  nchini,    mtandao huo   kupitia idara yake ya utafiti  na mafunzo  unasikitishwa  na  mikakati hafifu  ya Wizara ya Elimu  katika harakati za kutibu bomu zito la mfumo wa elime nchini.

“Ikumbukwe  kuwa   Julai 20 mwaka huu   TSNP  ilipeleka mapendekezo  wizarani kupitia waraka wake maalumu kuhusu muafaka wa  taifa  katika Mfumo wa Elimu Tanzania kwa Wizara ya Elimu 2016.’

“Lengo la waraka huu ni kuainisha  sababu  kuu mbili  kati ya sababu nyingine  zilizotolewa  na wadau wengi  wa elimu zilizosababisha mtandao wa wanafunzi  Tanzania  kuhubiri mapinduzi  ya mfumo wa elimu Tanzania.

 “Mfumo  huu tulionao sasa tumeurithi kutoka kwa wakoloni , hivyo basi tungependa mfumo wa elimu  urejee  kitabu cha UJAMAA  kilichoandikwa na hayati Mwalimu Nyerere  katika kurasa za elimu ya kujitegemea.

“Mwalimu  Nyerere alitilia shaka  kuhusu mfumo  wa elimu nchini  na hoja kuu aliyoitoa ni  ‘Urithi wa  elimu ya kikoloni’.

“Alikiri kuwa hakukuwa na mkoloni ambaye alikuwa na dhamira au shabaha  njema ya kumpa mwafrika elimu  kuunda mfumo mpya wa elimu utakaoakisi mazingira yetu,” walisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles