25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

KIGOGO NGORONGORO JELA MIAKA MITATU

Benard Murunya
Benard Murunya

Na JANETH MUSHI, ARUSHA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Arusha, imemtia hatiani Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Benard Murunya, kwa kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Kwa sababu  hiyo, mahakama hiyo imemhukumu kulipa faini ya Sh 700,000 au kwenda gerezani   miaka mitatu.

Murunya aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa NCAA na wenzake watatu, walikuwa wakishitakiwa kwa   matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 66,890 (Sh milioni 133.7).

Katika kesi hiyo namba 71 ya mwaka 2015, washtakiwa wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa  Fedha na Utawala wa NCAA, Shad Kiambile, aliyekuwa Meneja wa Huduma za Utalii katika mamlaka hiyo.

Wengine ni  Veronica Ufunguo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji wa Anga ya Cosmos Salha Issa, ambao waliachiwa huru na mahakama hiyo baada ya kupatikana hawana hatia.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Patricia Kisinda, alisema   katika kosa la kwanza   ilimtia hatiani Murunya kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Hakimu alisema Murunya alishindwa kuithibitishia mahakama kuwa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alimwagiza kubadilisha usafiri badala ya kupitia Kampuni ya Cosmos, wasafiri kwa Kampuni ya Antelop Tours.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles