28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

‘Wanafunzi wapewe mafunzo ya ukakamavu, uadilifu’

LUTENI Kanali Abubakari Charo
LUTENI Kanali Abubakari Charo

Na Harrieth Mandari,

LUTENI Kanali Abubakari Charo wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania (JKT), amesema utoaji mafunzo ya ukakamavu na maadili  kwa wanafunzi wanaojiunga elimu ya sekondari ni muhimu ili waweze kufanya kazi wanapohitimu masomo yao.

Hayo aliyasema jana wakati akifunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi 475 wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Jitegemee jijini Dar es Salaam.

Alisema ili kuendana na kauli mbiu ya awamu ya tano ‘Hapa kazi tu’ chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, ni muhimu kwa vijana kupata maandalizi hayo tangu wakiwa sekondari ili wajitambue, wenye uadilifu, uchapakazi na uaminifu miaka ijayo watakapokuwa watendaji katika sekta mbalimbali.

“Itakuwa vizuri iwapo shule zote zinazomilikiwa na jeshi la kujenga taifa nchini kuwa na mfumo wa aina hii ya mafunzo kwa wananfunzi ili kujenga taifa lenye vijana wakakamavu,” alisema na kuongeza:

“Ili Tanzania ya miaka ijayo iwe na taifa lililoendelea kuichumi, ni lazima kuanza kuwaandaa vijana sasa ambao ndio watendaji wajao.

Aliwatahadharisha wahitimu hao wa mafunzo kujikinga na majanga mbalimbali ikiwemo Ukimwi, matumizi ya dawa za kulevya na tabia zote hatarishi katika jamii.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo, Robert Kessy, alisema mfumo huo wa mafunzo kwa wanafunzi ulianzishwa miaka ya tisini ambapo hutolewa kwa wiku tatu hadi nne.

“Katika hiki kipindi cha mafunzo wanafunzi hao hupata elimu yao kama kawaida na ifikapo saa nane hufanya mafunzo hayo kwa saa moja na nusu kila siku hivyo kuwafanya vijana wetu kujiamini, kuwa watiifu na wakakamavu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles