26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wanne, mwalimu kortini kwa tuhuma za mauaji

Nyemo Malecela – BUKOBA

WANAFUNZI wanne, mwalimu pamoja na mlinzi wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic, wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Mood Muswadiku.

Wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji namba 18/2019 ni wanafunzi Husama Ramadhan (17), Sharifu Huled (19), Abdallah Juma (19) na Hussein Mussa (20), mwalimu Majaliwa Abud (35) na Badru Issa Tibagililwa (27) ambaye ni mlinzi.

Kesi hiyo iliyotajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Manispaa ya Bukoba, Frola Kaijage, imeahirishwa hadi Septemba 16, na watuhumiwa hawakutakiwa kujibu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kuisikiliza.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Chema Maswi, alidai mahakamani hapo kuwa mauaji hayo yalitokea Aprili 14, mwaka huu katika Shule ya Sekondari Katoro Islamic, Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera.

Watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi hadi kesi hiyo itakapokuja kutajwa tena kwa siku itakayopangwa na mahakama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles