27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Mbarawa amsweka ndani mkandarasi Kiteto

MOHAMED HAMAD-KITETO

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amemsweka rumande mkandarasi wa kampuni ya Kwilasa Invest Ltd, Bakari Abdala (48), kwa kujenga chini ya kiwango mradi wa maji wa Kijiji cha Kazingumu Kata ya Namelock wilayani Kiteto.

Shughuli za mradi huo zilikuwa ni kununua pampu ya kupandisha maji kwenye tanki, Ujenzi wa nyumba ya uzio wa mitambo ya pampu, Kulaza mabomba ya km tatu, Kujenga tanki la lita elfu 25 na kujenga vituo vinne vya kuchotea maji.

Akikagua mradi huo, Profesa Mbarawa alionyesha kutoridhishwa na ujenzi huo na kuagiza apatiwe kifaa cha kupigia hesabu (Kikokotozi) ambapo amesema kiasi cha Sh milioni 170 hakiendani na thamani ya mradi huo.

“DC huyu mtu ondoka naye mimi nitajuana na wataalamu wangu wa maji” alisema Waziri Mbarawa kisha mkandarasi huyo kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi

Naye Mbunge wa Jimbo la Kiteto Emmnuel Papiani (CCM), amesema miradi mingi Kiteto imekuwa ikichakachuliwa usimamizi mbovu na rushwa kwa baadhi ya watumishi wa Serikali na kusababisha malalamiko mengi kwa wananchi.

“Serikali ngazi ya Taifa, muendelee kufika hapa na kuwachukulia hatua hawa wakandarasi wasio waadilifu kwani wamekuwa kikwazo na hawachukuliwi hatua mpaka mje ninyi viongozi wa ngazi ya juu, hili kwangu halinifurahishi hata kidogo” Amesema Papian.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles