25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi waenda Finland kushiriki kongamano la mazingira

NA FRANCIS GODWIN, IRINGA

WANAFUNZI wawili wa Shule ya Southern Highlands Mafinga, Maria Wambura na Stephen Sang, wameondoka nchini kuelekea nchini Finland  kuiwakiisha Tanzania katika kongamano la mazingira la wanafunzi duniani.

Akizungumza wakati akiwakabidhi Bendera ya Taifa wanafunzi hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi, Festo Mgina, alisema heshima ambayo  shule hiyo imepata ni kubwa.

“Huu ni mwaliko wa heshima kubwa kwa wilaya yetu na mkoa, lakini kwa Taifa letu  kualikwa katika kongamano kubwa kama  hili la kujadili masuala ya mazingira  duniani, heshima hii sisi kama viongozi  tunajivunia na tunapongeza shule kwa   kuteuliwa kuwakilisha Taifa,” alisema. 

Aliagiza wakuu wa shule za msingi wilayani Mufindi kuhakikisha wanafika Southern Highlands ili kujifunza yale ambayo wanafunzi hao watarudi nayo.

“Tunataka elimu na maagizo ambayo yatatolewa katika mkutano huo wa dunia nchini Finland, vijana hao wakirudi basi  kuweza kusambaza kwa wenzao katika shule zote za Mufindi, ikiwa ni pamoja na wakuu wa shule kufika kujifunza ili kila shule kujifunza elimu hiyo kwa faida ya  mazingira ya maeneo yao,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Southern Highlands Mafinga, Kitova Mungai, alisema shule hiyo ni miongoni mwa shule wanachama wa Klabu za Mazingira Duniani na kuteuliwa kwa  wanafunzi hao kumetokana na ziara ya   waratibu wa kongamano hilo waliofika  kupima uwezo wa klabu zote nchini.

“Tunategemea kukutana na wawakilishi  kutoka nchi mbalimbali duniani kama China, Japan, Brazil, Marekani, China, Uganda, Kenya na nchi nyingine, ila tuna imani kubwa ya kuwakilisha vema Tanzania kwa sababu watoto waliochaguliwa kwenda katika kongamano  hilo wana uwezo mkubwa katika elimu ya mazingira,” alisema Mungai.

Alisema watoto hao na wenzao wamekuwa mbele kuhifadhi mazingira ya shule kwa kuotesha miche ya miti na kuipeleka shuleni hapo na nyumbani kwao.

Kwa upande wao, Maria na Stephen ambao ni wanafunzi wa darasa la saba, walisema kuteuliwa kwao katika  kongamano hilo si nafasi ya bahati mbaya kwa sababu wana uhakika wa kuliwakilisha  vizuri Taifa na kile watakachokipata  watakuja kukitumia kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles