28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai aitaka Simba kufanya makubwa zaidi

Na ZAINAB IDDY- DAR ES SALAAM

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameitaka klabu ya  Simba kuwa moja ya klabu kumi bora Afrika mwakani.

Ndugai aliyasema hayo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Mo Simba Awards 2019, zilizofanyika juzi usiku katika Ukumbi wa Hyatt Regency – The Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Ndugai, ambaye ni mwanachama wa Simba alisema mwaka huu timu hiyo imeonyesha mpira wa kiwango cha hali ya juu hivyo lazima mwakani wavuke malengo ya awali.

“Niwapongeze wachezaji kwa kazi kubwa waliyoifanya mwaka huu kwani wameweza kuiletea Tanzania sifa kimataifa baada ya kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini  niwatake viongozi na mwekezaji, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’,  kuhakikisha mwakani timu yetu inavuka malengo yaliyopita na kwenda mbele.

“Katika hili lazima waanze na kufanya usajili utakaoleta tija, bila kificho mwaka huu hatukuwa na safu nzuri ya ulinzi hivyo lazima waanze kuibomoa nafasi hiyo na kuleta bora zaidi ili kuyavuka malengo ya mwaka huu nina hakika hili linawezekana,” alisema na kuongeza:

 “Baada ya usajili makini kazi ibaki kwa wachezaji na benchi la ufundi wanaotakiwa kuhakikisha wanapambana kadiri wanavyoweza ili kupata ushindi uwanjani, binafsi nitaendelea kuwa bega kwa bega kwa kila hatua mtakayopita.” 

Katika hafla hiyo, mshambuliaji, Meddie Kagere, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo, pia alichukuwa tuzo ya mfungaji bora, wakati John Bocco, alichaguliwa kuwa mshambuliaji bora,  Erasto Nyoni, alichaguliwa kuwa beki bora wakati kiungo bora ni James Kotei, kipa bora Aishi Manula, wakati mchezaji mdogo aliyefanya vizuri msimu huu akichaguliwa Rashid Juma.

Mchezaji aliyefunga bao bora ni Clatous Chama, tuzo mpya ya mchezaji aliyechaguliwa na wenzake ni Erasto Nyoni, Azim Dewji alipewa tuzo ya heshima kwa klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles