24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi waandamana kutaka walimu waongezewe mshahara

MAMIA ya wanafunzi wa shule za umma kutoka Beni na Kinshasa wameandamana nchini DR Congo, wakitaka walimu wao waongezewe mshahara.

Wanafunzi hao walifanya maandano hayo jana, wakidai wanataka kusoma kutokana na walimu kuwa na mgomo tangu Oktoba 4, 2021, wakishinikiza kuongezewa mshahara na kupunguza umri wa kustaafu pamoja na masuala mengine. 

Katika maadhamano hayo, wanafunzi hao walikuwa  wanaimba kuwa “tunataka kusoma” na “ikiwa hatutasoma, tutatumia dawa za kulevya”.

Radio inayomilikiwa na Umoja Mataifa- Radio Okapi, imeripoti kuwa maandamano yamekuja baada ya wazazi wa wanafunzi haoa Jumatatu iliyopita kueleza  hasira zao  kwenye Wizara ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Elimu ya Ufundi (EPST).

Wazazi hao walisema wamechoka kupeleka watoto wao shule bila kusoma.

Makamu wa rais wa DR Congo, Jean-Marc Kabunda, amewataka wanafunzi kurudi nyumbani kwa sababu si  mapambano yao.

Waziri wa Wizara ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Elimu ya Ufundi (EPST). DR Cong, Tony Mwaba

“Nyinyi sio watu wa mtaani, mnapaswa kuwa shuleni na kama hampo shule mnapaswa kuwa nyumbani,” amesema.

Hata hivyo saa chache baada ya maandamo hayo, Waziri wa EPST, Tony Mwaba, aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa hakuna chama cha walimu kilichoamuru mgomo huo kwa njia ya kisheria na rasmi na kutangaza  kuanza tena kwa mazungumzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles