25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wa kike Iringa watakiwa kupiga vita anasa

RAYMOND MINJA – IRINGA

Naibu katibu Mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania bara(UWT),  Jeska Mbogo, amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa kuelekeza akili zao na nguvu zao kwenye masomo badala ya kuzipeleka kwenye mambo ya  anasa.

Mbogo ameyasema hayo leo Juni 18, wakati akizunguza na wanafunzi  wa vyuo vikuu vinne  ambao ni wanachama wa UWT ambapo amewakabidhi rasmi kadi za jumuiya hiyo na kuwataka wajikubali jinsi walivyo na kuachana na tabia ya kujibadilisha maumbile kwa kutumia dawa za kachina.

“Ndugu zangu kitu cha kwanza kwenye Maisha yako kama mwanafunzi ni kujitambua jua umefuata nini chuoni acheni kujirahisisha mnatumika sana ,wengine mnajibebisha kwa walimu wenu ili muweze kuongezewa alama kwenye mitihani yenu achene  kujirahisisha vivyo nye ni dhahabu subirini muda wenu  ufike,” amesema.

Aidha amewataka wazazi kutenga muda wa kuwa karibu na watoto wao na  kuzungumza nao  kwani wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta fedha na kuwasahau watoto wao jambo ambalo linazidisha mmomonyoko wa maadili kwa watoto wengi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve amewataka vijana hao kujiamini katika Maisha yao na kutokuwa watu wakulaumu na kulalamika bali wawe ni watu wa kufanya kazi kwa vitendo kulisaidia Taifa lao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles