28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

IFM kuhamishia kozi za cheti, stashahada simiyu

Derick Milton – Simiyu

Uongozi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), umesema kozi zinazotolewa na chuo hicho ngazi ya cheti na stashahada katika tawi lake mkoani Mwanza zitahamishiwa kwenye tawi la Simiyu mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Juni 18, na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Thadeo Sata wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa tawi la chuo hicho Mkoni Simiyu iliyofanyikia katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi, ambapo amesema kuwa tawi la Mwanza litaendelea kufundisha kozi za ngazi za juu zaidi shahada, na shahada ya uzamili ambazo zinatawapa fursa wafanyakazi kusoma jioni.

“Tunategemea chuo hiki tawi la Simiyu ujenzi wake ambao uko chini ya VETA utakamilika mwezi Septemba, baada ya kukamilika wanafunzi walioko mwanza ngazi ya cheti na deploma watahamishiwa hapa,” amesema Prof. Sata.

Aidha amesema kuwa mkandarasi atafanya kazi usiku na mchana ili chuo hicho kianze kazi mara moja na kuweza kuwanufaisha wakazi wa mikoa ya shinyanga, Simiyu, Mara na Geita huku ujenzi wake ukigharimu kiasi cha shilingi Milioni 971.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kuwa kukamilika kwa chuo hicho, kutaongeza chachu ya maendeleo katika mkoa wa Simiyu na kuwa fursa kubwa kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles