27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi ualimu wamlilia JK ukosefu wa ajira

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete
RAIS mstaafu Jakaya Kikwete

NA RAYMOND MINJA – IRINGA

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amewatoa hofu wahitimu wa shahada za ualimu, kuwa wasikatishwe tamaa na tatizo la ajira nchini kwani suala hilo ni la mpito na litakwisha muda si mrefu.

Kikwete aliyasema hayo jana alipokuwa akiwajibu wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa mjini hapa, walioonyesha wasiwasi wao kuhusu tatizo la ukosefu wa ajira nchini na kutaka Serikali ilipatie ufumbuzi ili wanapohitimu wawe na uhakika.

Wahitimu hao walipaza sauti wakimsihi Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika mjini hapa, azungumze na Rais Dk. John Magufuli ili afungue milango ya ajira katika sekta hiyo la sivyo watakufa kwa njaa.

“Inaumiza kuona wenzetu waliomaliza chuo hicho mwaka mmoja uliopita wakiendelea kusota mitaani bila ya kuwa na kibarua chochote, na sisi tunaamini tutaungana nao kuisoma namba,” alisema mmoja wa wahitumu hao ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Akijibu, Kikwete alisema “ujumbe umefika”.

Aliwatia moyo wahitimu  952 aliowatunuku vyeti vyao katika fani nne za shahada za elimu, kuwa  tatizo la uchelewaji wa ajira litakwisha baada ya muda mfupi kwani taifa lina uhitaji mkubwa wa walimu katika masomo mbalimbali.

Kikwete aliyetumia takribani dakika tatu kuzungumza na wahitimu hao wakati akifunga mahafali hayo, alisema ataufikisha ujumbe huo kunakohusika kama alivyoombwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles