26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI 650,000 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI),  Selemani Jafo

 

Na SARAH MOSES-DODOMA

WANAFUNZI 650,862 (asilimia 98.31), wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu.

Vilevile, Serikali imetoa wiki mbili kwa wanafunzi hao kuripoti shule walizopangiwa na kama wakichelewa   nafasi zao watapangiwa  wanafunzi wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dodoma jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI),  Selemani Jafo alisema ufaulu huo ni  a ongezeko la wanafunzi 124,209 ikiwa ni sawa na asilimia 23.58.

Jafo alisema   mwaka huu wanafunzi 1,912 wenye mahitaji maalumu waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga   kidato cha kwanza mwakani.

Alisema  wanafunzi 11,173 (asilimia 1.69 ya waliofaulu) hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga   kidato cha kwanza katika awamu hiyo ya kwanza ya uchaguzi.

“Sababu iliyosababisha  wanafunzi hao kutokuchaguliwa  ni uhaba wa miundombinu ya elimu vikiweamo vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya halmashauri,” alisema Jafo.

Aliitaja mikoa ambayo halmashauri zake zimeshindwa kuchagua wanafunzi kuwa ni Lindi wanafunzi (170), Mbeya (3,092),  Rukwa  (4,091), Manyara  (1,268),  Katavi (976)  na Simiyu ( 1,576).

Waziri aliwataka wakuu wa mikoa iliyotajwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza  mwaka 2018.

“Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wanatakiwa kuripoti shuleni Januari 18, 2018,” alisema Jafo.

Alisema mikoa ambayo ina tatizo la miundombinu ni lazima ikamilishe miundombinu hiyo haraka   wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya Februaru 15  mwakani.

Hata hivyo Jafo amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kutumia fursa hiyo vizuri katika kujifunza na kuachana na anasa au starehe ambazo zitawafanya kupata matokeo mabaya   kidato cha nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles