25.6 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

DK. SHEIN AAPISHA WAKUU WA MIKOA

Na MWANDISHI MAALUM-ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha wakuu wa mikoa wapya na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto (anayeshughulikia masuala ya Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto).

Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ikulu ya  Zanzibar.

Waliopishwa ni Hassan Khatib Hassan ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hemed Suleiman Abdallah, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba na Mwanajuma Majid Abdallah, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto.

Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Said Hassan Said, mawaziri na manaibu waziri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,504FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles