24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 120 kushiriki Umitashumta Dar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanafunzi 120 kutoka shule mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamechaguliwa kuunda timu itakayovaana na halmashauri nyingine kwenye mashindano ya Umitashumta ngazi ya mkoa.

Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Msingi Mzambarauni, Maria Mawata, akitambulisha timu ya wanafunzi viziwi kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji BoT, Kened Nyoni, wakati wa kufunga mashindano ya umitashumta ngazi ya jiji yaliyofanyika Uwanja wa Kabby Pugu Kinyamwezi. Katikati ni Kaimu Afisa Michezo Jiji la Dar es Salaam, Asha Mapunda.

Timu hiyo inajumuisha wachezaji wa soka, soka maalumu, wavu, mikono, pete, kwaya, ngoma na riadha.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Umitashumta Kaimu Afisa Michezo wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Asha Mapunda, amesema wanafunzi hao watakaa kambini kwa siku 10 hadi Julai 14 kwa ajili ya kujiandaa kushiriki mashindano ngazi ya mkoa.

“Mwaka jana tulitoa wanafunzi 72 katika timu ya mkoa iliyokwenda kwenye mashindano ya taifa, matarajio yetu kwa mwaka huu ni kuwa mabingwa wa michezo yote,”amesema Mapunda.

Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Abilahi Mchiha, amesema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya michezo mbalimbali na kutambua wanamichezo mahiri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye alimwakilisha gavana katika kufunga mahsindano hayo, Kened Nyoni, amewapongeza wanafunzi waliochaguliwa kuunda timu ya halmashauri na akawataka waongeze bidii watakapokuwa kambini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles