23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanachama, Mashabiki wa Simba Chamwino wachangia damu

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KUELEKEA kilele cha Simba Daya kinachofanyika leo Jumapili Septemba 19, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam, Wanachama, Wapenzi na Mashabiki Simba SC Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamechangia damu, kufanya usafi  pamoja na kuwafariji wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chamwino huku wakiuomba uongozi wa timu hiyo kulipeleka tamasha hilo mikoani ili mashabiki wapate nafasi ya kuwaona wachezaji.

Wakizungumza na Mtanzania Digital Septemba 18, katika Hospitali hiyo, mashabiki hao wameuomba uongozi wa timu hiyo kulipeleka tamasha hilo mikoani ili waweze kupata nafasi ya kuwaona wachezaji wa timu hiyo pamoja na timu hiyo kujiongezea kipato.

Mwanachama wa timu hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Buigiri na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino, Kenneth Yindi amesema Simba ni timu kubwa hivyo inahitaji kuendelea kufanya mambo makubwa kama ambavyo inafanya sasa hivyo kwa kuongeza wigo wa mashabiki kuiona timu yao.

Yindi amesema wameamua kuanzisha kikundi cha Jogging cha mashabiki wa timu hiyo  na  kutoa damu,kuwafariji wagonjwa pamoja na kuchangishana fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gifti Msuya katika kampeni yake ya nishike mkono ambayo ina lengo la kuchangia ujenzi wa madarasa,matundu ya vyoo na madawati ili wanafunzi waweze kusoma.

“Sisi hapa Ikulu tumeamua kwenda pamoja na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mazoezi ya pamoja,pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa lakini pia tumefanya usafi hii ni Simba timu kubwa timu yenye maono ya mbali, timu yenye muda wote inaleta furaha,” amesema Yindi.

Kwa upande wake, Katibu wa tawi la Simba Wilaya ya Chamwino, Fatna Ibrahim ameuomba uongozi wa timu hiyo kuangalia utaratibu wa uuzaji wa tiketi kwani wanachama wamekuwa wakikutana na wakati mgumu wakati wa kununua tiketi.

Naye, Emmanuel Lotto, Philbert Mazige na Matimba John wameiombea kila la heri timu hiyo katika mchezo wa kesho dhidi ya TP Mazembe ya Nchini Congo  mtanange  unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles