22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti BAWACHA Dodoma ahamia CCM

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA) Mkoa wa Dodoma, Eva Mpagama amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi na miradi mikubwa  iliyoachwa na marehemu Dk. John Magufuli.

Akizungumza Septemba 18, mara baada ya kumkabidhi kadi ya Chadema Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga, Mpagama amesema amejiunga na chama hicho kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya marehemu Magufuli kwa jinsi ambavyo alitekeleza miradi mingi ambayo mpaka sasa inaendelea kukamilika.

“Nisiwe muongo nimekuja CCM sababu ya Magufuli (marehemu) ameitendea haki nchi hii kila sehemu kumetifuliwa kuna ujenzi unaendelea, nimekaa nimejitafakari nimeona nije CCM kuendeleza yake mazuri ambayo yamefanya na nina imani Rais wa sasa anaendelea kuyatekeleza yale mazuri ambayo yamefanywa,” amesema.

Mpagama amesema sasa anajipanga kuendelea kukipigania Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha yale mazuri ambayo yanaendelea kufanya na Chama hicho yanasemwa ili kila mmoja aweze kufahamu.

Kwa upande wake,Katibu wa CCM,Mkoa wa Dodoma,Pili Mbaga alimpongeza Eva kwa kujiunga na CCM ambapo amedai uamuzi aliofanya ni mzuri na alichelewa.

“Huku ndio kila kitu sisi tunamkaribisha kwa mikono miwili na sasa aende katika eneo lake ili aweze kupatiwa kadi ya uanachama,CCM Mkoa wa Dodoma  itaendelea kuhakikisha inaendelea kumuunga mkono Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles