29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki wa kampuni za biashara waaswa kutangaza utalii wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ametoa wito kwa Wafanyabiashara na wamiliki  wa Makampuni mbalimbali hapa nchini kuunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza Utalii  na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini kupitia biashara zao.

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mary Masanja akiwaasa wamiliki wa Kampuni za Biashara nchini kutumia fursa hiyo kuutangaza Utalii wakati wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika Mei 2, 2021 jijini Mwanza.

Mary Masaanaja ametoa wito huo jana Jijini Mwanza, wakati wa maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayowahusisha wadau mbalimbali. Amesema wafanyabiasha ni wadau wakubwa wa utalii hivyo wana nafasi kubwa ya  kuutangaza utalii hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya Watalii.

“Nawaomba sana ninyi wafanyabiashara,  kupitia makampuni yenu mtangaza Utalii wa Tanzania na vivutio vyake  ,ninyi ni wadau wakubwa wa utalii,”amesema Masanja.

Amewaeleza  wafanyabiashara hao kuwa wanapaswa kutambua kuwa Sera ya Tanzania ya Viwanda itaendelea kutekelezwa kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekua akiwasisitiza Watanzania  wawekeze katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo amesema wafanyabiashara wakishirikiana vizuri wataweza kukuza uchumi wa nchi pia kuutangaza utalii.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali ikiwemo uondoaji wa  urasimu na ukiritimba kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza hapa nchini.

“Serikali tunaendelea kuziondoa changamoto kuziondoa changamoto zote zinazolalamikiwa na wafanyabiasha na wawekezaji,tuvute subira kidogo haya mambo yatakwenda kurekebishwa vizuri,”amesema Mashimba

Hata hivyo, amezitaka Mamlaka za Serikali za mitaa kutengeneza wafanyabiashara watakaolipa mapato kwa kuwapatia maeneo watakayo fanyia Biashara Ili waweze kulipa kodi na kukuza uchumi wa nchi .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles