26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wambura: Sitambui kufutwa uanachama

Michael Wambura
Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Michael Wambura,

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MWANACHAMA wa Simba, Michael Wambura, amesema hatambui uamuzi wa mkutano mkuu wa klabu hiyo kumfuta uanachama yeye na wanachama wengine, akidai uamuzi huo unapingana na Katiba ya Simba na ile ya nchi.

Agosti 3, mwaka huu, Mkutano Mkuu wa Simba ulimfuta uanachama Wambura na wanachama 71 waliopeleka kesi ya uchaguzi mahakamani, suala hilo linalokinzana na Katiba ya Simba ibara ya 55, ambayo inaonyesha wazi kuwa mwanachama atakayekuwa amepeleka kesi mahakamani atakuwa amejifuta uanachama hadi mkutano mkuu utakapoamua.

Wambura amepewa adhabu hiyo kutokana na kuifungulia kesi Simba katika Mahakama ya Kisutu mwaka 2010, huku wanachama wengine wakipewa adhabu hiyo kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani mwaka huu, wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Wambura alisema uamuzi huo haujafuata katiba ya nchi ibara ya 13 (1) a, ibara ya 35 (1) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ibara ya 54 (4)(5) ya Katiba ya Simba, ambazo zinaonyesha kuwa huwezi kumhukumu mtu bila kumpa nafasi ya kujitetea, hivyo walipaswa kupewa barua ya kuwatuhumu na wao wajitetee kabla ya kutoa uamuzi huo.

“Lakini ibara ya 54 (3) ya Katiba ya Simba inasema hoja yoyote lazima ipigiwe kura ya siri baada ya kujitetea na ikifikia theluthi ya wapiga kura ndiyo maamuzi yapitishwe, hii haijafanyika, hivyo mwamuzi hajatenda haki na ninawaambia wanachama waliofukuzwa wana haki ya msingi ya kuendelea kupigania haki yao,” alisema.

Alisema hadi sasa hajapewa barua ya kufukuzwa uanachama, anawaomba wampe barua hiyo haraka na tayari amewasiliana na wanasheria wake kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi, kwa kuwa hakubaliani na uamuzi huo, kwani wanachama wa hivi karibuni hawawezi kuwafuta wanachama ambao ni waanzilishi wa Simba.

“Siyo kama napigania uanachama kama kuna kitu nataka Simba, lakini kukubali kufutwa uanachama ni sawa na kutenda dhambi ambayo nitakuwa sijaitendea haki Simba na hata nchi yangu, lazima nipambane kupata ufafanuzi wa katiba hizi,” alisema.

Aliongeza kuwa anashindwa kuelewa kesi iliyotumika kumpa adhabu hiyo, akijiuliza ni ile ya 2010 ambayo aliipeleka Simba mahakamani au ya 2014 , ambayo wanachama wameipeleka Simba mahakamani, yote anahitaji kupata ufafanuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles