23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Walk it Off ya Fid Q yashinda video bora ya Ziff

Farid Kubanda ‘Fid Q’
Farid Kubanda ‘Fid Q’

NA FESTO POLEA, ZANZIBAR 

TUZO mpya ya video bora ya wimbo wa Bongo Fleva imekwenda kwa Farid Kubanda ‘Fid Q’ kupitia video ya wimbo wake wa ‘Walk it Off’.

Katika shindano hilo, wasanii saba wa muziki wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam na watatu kutoka Uganda walioshindanishwa video zao, video hiyo ndiyo iliibuka mshindi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando, Fid Q atakuwa balozi wa tamasha hilo kwa mwaka mzima na ataandaa wimbo wa tamasha hilo kwa mwaka ujao.

“Video hiyo ndiyo iliyochaguliwa kuwa bora na majaji wetu, msanii wa video hiyo ndiyo balozi wetu kwa mwaka mzima, naye ndiye atatunga na kurekodi wimbo wa Ziff kwa tamasha lijalo,” alisema Profesa Mhando.

Baadhi ya video zitakazoshindanishwa ni pamoja na ‘Aje’ wa Ali Kiba, ‘Sweet sweet’ wa Chege Chigunda, ‘Zigo Remix’ wa Ay aliomshirikisha Diamond Platnumz na ‘Sizonje’ wa Mrisho Mpoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles