Filamu ya Aisha yaongoza Tuzo za Ziff

Muongozaji Aisha na prodyuza wake
Muongozaji Aisha na prodyuza wake
Muongozaji Aisha na prodyuza wake

FILAMU ya Aisha imenyakua tuzo nne za Ziff ikiwemo mwigizaji bora wa kike, Godliver Gordian, mhariri bora wa video, Momose Cheyo, mwongozaji bora, Chande Omari na filamu bora ya makala iliyokwenda kwa prodyuza, Amil Shivji. 

Tuzo hizo za Bongo Movie zimetolewa kwa vipengele viwili kikiwemo cha tuzo za Azam na tuzo za ComNet.

Filamu nyingine zilizoshinda tuzo ni filamu ya ‘Kariakoo’, iliyoshinda tuzo ya filamu yenye picha nzuri ambayo imeongozwa na Freddy Feruzi.

Nyingine ni tuzo ya muigizaji bora wa kiume iliyokwenda kwa Salim Ahmed ‘Gabo’, kupitia filamu ya ‘Safari ya Gwalu’, nyingine ni tuzo ya mwandishi bora iliyokwenda kwa Abubakar H. Guni na Devotha Mayunga wa filamu ya ‘Queen of Masai’.

Tuzo ya filamu yenye sauti bora imekwenda kwa  filamu ya ‘Bongo na Flava’, iliyoandikwa na Joseph Myinga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here