24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

WALIOKUWA RAIA WA BURUNDI WATAHADHARISHWA

Na Walter Mguluchuma

– Katavi

SERIKALI imewaonya Watanzania wapya waliokuwa  raia wa  Burundi wakatakaobainika kujihusisha na uhalifu ikiwamo kufanya mazoezi  ya kivita, ujangili, ubaguzi wa kikabila na dini kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwao.

Onyo hilo lilitolewa na Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara  kwa Watanzania hao wapya wanaoishi katika makazi ya Katumba.

“Wapo baadhi yenu ambao mmeshakubaliwa na kupewa uraia wa nchi hii, zipo taarifa kuwa mnajihusisha na uhalifu  ukiwamo ujangili katika hifadhi, pia mna ubaguzi wa kikabila ambapo mnawahamasisha wenzenu wasinunue bidhaa kwenye maduka ya wafanyabiashara wazawa hii haiwezi kukubalika.

“Wenyewe kwa wenyewe mnabaguana kwamba wengine mnatoka milimani na wengine chini ya milima mkidharauliana kwamba upande mmoja ni bora kuliko mwingine, huu si utamaduni wetu Watanzania,” alisisitiza.

Aidha, waziri huyo aliwataka raia hao wapya kuwa wazalendo huku akisisitiza kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya kuwapatia uraia ambapo mpaka sasa  kuna vyeti vya uraia vipatavyo 7,551 ambavyo  havijachukuliwa licha ya wakimbizi walioomba kukubaliwa.

Alisema Serikali haiwezi kuondoa   utaratibu wa watu kuingia  kwenye   makazi hayo bila mtu kuwa na kibali   mpaka  hapo itakapokuwa imejiridhisha kuwa watu wanaoishi kwenye maeneo  hayo watakuwa wameacha vitendo vya uhalifu.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Raphael Muhuga, aliwataka wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo ya Katumba ambao wanataka kurejea Burundi, wawe huru  kwani milango iko wazi, jambo la muhimu wazingatie utaratibu.

Aidha, Muhuga aliwataka raia hao kuendelea kutunza mazingira kama  ambavyo walivyokuwa wakiyatunza kabla ya kuwa raia rasmi.

Wakati huo huo raia hao wamemuomba Mwigulu kuyafuta baadhi ya madhebu ya dini  yaliyopo katika makazi hayo ambayo yanachochea ubaguzi wa dini.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Yusuf Shaabani alimweleza Waziri Nchemba kuwa ubaguzi wa dini umekithiri kwenye makazi yao, ambapo hata kuoana waumini wa madhehebu tofauti wanakataliwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Makazi ya  Wakimbizi ya Katumba, Athuman  Ingwe, alieleza  kuwa makazi  ya  Katumba  yalianzishwa  mwaka 1973 na yana watu 78,201 kwa sasa, huku raia  wapya wakiwa ni asilimia 98 na waliobaki bado ni  wakimbizi wa  Burundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles