30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBACHAWENE AIMWAGIA SIFA SIMANJIRO

Na BEATRICE MOSSES-MANYARA

WAZIRI wa Tamisemi, George Simbachawene, amezitaka wilaya nyingine nchini kuiga Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kwa kuwa wilaya hiyo imejenga majengo mazuri ya madarasa, maabara na nyumba za walimu.

Simbachawene aliyasema hayo jana kwenye ziara yake ya siku moja wilayani Simanjiro, baada ya kufika katika Shule ya Sekondari Loiborsiret iliyoko wilayani humo.

“Majengo ya Simanjiro yamejengwa vizuri kwa sababu yamesimamiwa vizuri na kujengwa kwa ubora unaotakiwa.

“Kwa hiyo, viongozi wa wilaya nyingine nchini wanapaswa kupata somo kupitia ujenzi huo ambao thamani ya fedha inaendana na thamani ya ujenzi wa miundombinu iliyofanyika.

“Nasema hivyo kwa sababu baadhi ya maeneo, viongozi wanashindwa kusimamia ili yajengwe majengo bora yanayodumu.

“Pamoja na hayo, nawapongeza pia wanafunzi wa shule hii ambao wengi wao ni jamii ya kifugaji wa kimasai, kwani baadhi yao nimekagua madaftari yao na kubaini kiwango cha taaluma ni kizuri tofauti na matarajio yangu.

“Kwa hiyo, walimu wa shule hii wanastahili pongezi nyingi kwa kufanya kazi yao kwa uadilifu na pia wanafunzi nao kwa upande wao wanatakiwa kupongezwa kwa sababu wanatimiza wajibu wao ipasavyo,” alisema Simbachawene.

Naye Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Martin Mwashambwa, alisema ujenzi huo umegharimu Sh milioni 219.9.

“Ujenzi huo umehusisha nyumba kubwa yenye uwezo wa kuishi familia sita iliyogharimu shilingi milioni 149.9 na vyumba viwili vya madarasa vya thamani ya shilingi milioni 49.6.

“Ujenzi mwingine ni wa vyoo vya wanafunzi wa shule hiyo uliohusisha matundu manane yenye thamani ya shilingi milioni 20. 3,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles