22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

ATCL KUBORESHA HUDUMA ZA NDEGE ZANZIBAR

Na MWANDISHI WETU

-ZANZIBAR

SERIKALI imesema Shirika la Ndege nchini (ATCL), litaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri wa anga katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha Kamati ya Mawasiliano na Ardhi ya Baraza la Wawakilishi (BLW) na uongozi wa Shirika hilo,  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, alisema kuwa changamoto ambazo wameziwasilisha katika kikao hicho zitafanyiwa kazi ili kuleta tija kwa pande zote mbili.

“Nawahakikishia wajumbe wa kamati hii kuwa changamoto mlizonazo tutazifanyia kazi haraka kwani ATCL sasa imezaliwa upya na hivyo itahakikisha inaboresha masilahi ya kuliinua na kuliendeleza shirika ili kuweza kukidhi mahitaji ya hapa na visiwani,” alisema Ngonyani.

Alisema katika kuhakikisha huduma za usafiri wa anga visiwani humo zinaimarika, tayari Serikali imeshaanza kulipa deni lililokuwa linadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege la Sh milioni 241 ambalo shirika hilo linadaiwa kutokana na tozo ya maegesho ya ndege na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamza Juma, alimwomba Naibu Waziri Ngonyani kuangalia upya suala la ajira ATCL ili liweze kubeba sura ya Muungano na kuwawezesha wataalamu wenye sifa kutoka Zanzibar nao kupata nafasi hizo.

“Tunaomba Shirika na baadhi ya taasisi zinazofanya kazi kwa kushabihiana na masuala ya Muungano kuzingatia utoaji wa ajira katika nafasi wanazozitangaza kwani Zanzibar ina wataalamu wenye sifa lakini hawapati fursa,” alisema Hamza.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Emmanuel Korosso, alisema Shirika hilo linaendelea kuimarika na kusambaza huduma katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini licha ya kuwa na changamoto za uhaba wa marubani

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles