29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WALICHOTETA JPM, BABU SEYA IKULU


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, amekutana na mwanamuziki Nguza Viking maarufu Babu Seya na watoto wake Ikulu, Dar es Salaam.

Mwanamuziki huyo na watoto wake, walikwenda Ikulu jana kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwaachia huru kwa msamaha yeye na mtoto wake Johnson Nguza, maarufu ‘Papii Kocha’ waliokuwa wakitumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Katika mzungumzo yake na mkuu huyo wa nchi, Babu Seya na Papii Kocha walimshukuru kwa msamaha alioutoa kwao na wafungwa wengine 61 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo na walimuahidi watakuwa raia wema na watachapa kazi kwa juhudi na maarifa.

Babu Seya pia aliambatana na watoto wake wengine Nguza Mbangu na Francis Nguza.

“Yaani sijui nisemaje, hapa nina furaha kubwa sana moyoni mwangu, nilikuwa naomba sana tangu muda mrefu nikutane nae, nimeomba sana sana, hatimaye leo (jana) nimefanikiwa na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na sasa nipo tayari kuchapa kazi, Hapa Kazi Tu,” alisema Nguza na kuungwa mkono na mwanae Papii.

Katika mazungumzo hayo, Nguza na wanae walimwombea Rais Magufuli na walimweleza kwa sasa wanajipanga kuendeleza kazi zao za sanaa.

Kwa upande wake, Rais Magufuli, aliwashukuru kwa kwenda kumwona na kumshukuru, lakini akasema …………………………

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles