24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WALIA KUUZIWA MBEGU FEKI ZA VITUNGUU

vitunguu

Na LUPAKISYO KINGDOM, MBARALI

WAKULIMA wa vitunguu katika skimu ya umwagiliaji ya Kijiji cha Igawa, Kata ya Lugelele wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wamelalamikia baadhi ya kampuni zinazozalisha mbegu za zao hilo kwa kuwauzia mbegu feki na kusababisha kuzalisha mazao yaliyo chini ya kiwango na hivyo kukosa soko.

Wakizungumza na MTANZANIA jana walisema mbali na uzalishaji wa vitunguu kushuka, kitendo hicho kimewaondolea uaminifu kwa baadhi ya kampuni.

Mmoja wa wakulima hao, Raphaely Mbendo, alisema: “Kuna paketi za mbegu za vitunguu kutoka kwa baadhi ya kampuni zinaonyesha picha ya vitunguu vyekundu ambavyo soko lake linapatikana mahali popote ndani na nje ya nchi lakini vinapopandwa vinatoa rangi nyeupe tofauti na matarajio yetu,” alisema Mbendo.

Naye mjumbe wa Bodi ya Ushirika wa wakulima wa vitunguu katika skimu hiyo, Pascal Zawadi, aliwataka viongozi wa kampuni za uzalishaji wa mbegu za vitunguu nchini kuwatembelea mawakala wa uuzaji wa mbegu hizo na kuzikagua ili kubaini watu wanaozichakachua kwa manufaa yao.

“Inaonekana wazi kuwa mchezo huu wa ubadilishaji wa mbegu za vitunguu unafanywa na baadhi ya watu kutoka nje ya kampuni ya uzalishaji na si kampuni yenyewe  hivyo tunayaomba makampuni yawe yanafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa wauzaji wa mbegu hizo ili kuwabaini watu wanaochakachua na kuwachukulia hatua za kinidhamu pale wanapopatikana,” alisema Zawadi.

Aidha, Zawadi alisema endapo ukaguzi utafanyika kila mara wale wanaowahujumu wakulima kwa kuwauzia mbegu feki zisizo na ubora watabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles