30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WAHIMIZWA KILIMO CHA MKATABA

 

Na FREDRICK KATULANDA

WAKULIMA wa pamba nchini wamehimizwa kujiunga na kilimo cha mkataba kwa kuwa kina faida na mafanikio kwao na taifa kwa ujumla.

Meneja wa Kanda wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Jones Bwahana, alisema kilimo cha mkataba kimesaidia kuongezeka   eneo la kilimo cha pamba na matumizi ya mbegu bora mpya isiyo na manyoya ya aina ya UK M08 inayozalishwa na kiwanda cha Quton (T) Ltd.

Alisema kilimo hicho kimesaidia katika kusambaza haraka na matumizi ya viuadudu  na upatikanaji wa huduma za ugani kwa wakati kwa wakulima hali ambayo imeongeza ufanisi wa kilimo na tija hivyo kukuza uzalishaji wa pamba.

“Katika kilimo cha mkataba mkulima analipa akiwa na makubaliano na kampuni anayoingia nayo mkataba ambayo itampatia mbegu bora za kilimo aina ya UKM 08 isiyo na manyoya, dawa za kuulia wadudu kwa mkopo na huduma za ugani bure, makulima akivuna hurejesha mkopo kwa kampuni.

“Kilimo hiki kimewafanya wakulima wa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora, Kagera, Kigoma na Singida kupata usimamizi mzuri wa sheria na sera za kilimo kupitia maofisa ugani,” alisema.

Alisema awali wakulima walilalamikia mbegu hiyo kutoona lakini   sehemu kubwa ya wananchi hao walikuwa wakipanda bila kufuata maelekezo ya maofisa ugani.

Alisema  baada ya kupewa elimu na kusimamiwa vema sasa wameelewa matumizi sahihi ya mbegu hizo na kuzalisha kwa ufanisi.

“Kwa sasa pamoja na kwenda vizuri, kuna changamoto ambayo bodi ya pamba inaendelea kukabiliana nayo.

“Tunatoa elimu ya kilimo cha mkataba ambako tunawaelimisha namna ya kulima kwa kuzingatia vipimo na maelekezo yanayopendekezwa na wataalamu   na kuacha kuchanganya pamba na mahindi,” alisema.

Mkaguzu wa Mbegu wa Kampuni ya Quton, Wilbert Boniface alisema tatizo la wakulima katika kilimo walikuwa wakilima kwa mazoea wakipanda   huku wakichanganya pamba na mazao mengine.

“Tumekuwa tukiwaelimisha kutochanganya mbegu, hivyo kama mkulima ana shamba la ekari mbili tunamhumiza apande pamba ekari moja na nyingine mazao mengine.

“Wamefuata na sasa wanapanda pamba kwa kufuata mstari kwa vipimo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles