25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

WANAUME 20 WAKAMATWA KWA MIMBA ZA WANAFUNZI

Na IBRAHIM YASSIN-NKASI

WANAUME 20 wamekamatwa wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, kwa tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi.

Kutokana na hali hiyo, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya taratibu zote kukamilika.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda, katika mikutano mbalimbali ya hadhara katika vijiji vya Mandakelenge na Kipili, Kata ya Kipili.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, wilaya yake iko katika vita ya kupambana na mimba shuleni na kwamba operesheni hiyo ni endelevu kwa kuwa lengo lao ni kukomesha vitendo hivyo.

“Wanafunzi wengi wa kike wamekuwa hawamalizi masomo kwa sababu ya mimba. Ili kuwaokoa, tumeamua kuanzisha vita ya wilaya na hata wale waliokimbia baada ya kujua tunawatafuta kwa makosa ya kuwatia mimba wanafunzi, tutaendelea kuwasaka hadi tutakapowakamata.

“Kwa hiyo nawataka wanaume wenye kawaida ya kufanya mapenzi na watoto wa shule, waache tabia hiyo kwa sababu tukiwajua, tutawakamata na kuwafikisha mahakamani kama tunavyotarajia kufanya kwa hawa 20 tuliowakamata tayari,” alisema Mtanda.

Pamoja na hayo, Mtanda alilalamikia tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuharibu ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa na kuwa jambo hilo nalo wameanza kupambana nalo ili wanaume hao wachukuliwe hatua.

“Katika hilo, hivi karibuni tulimkamata Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwai ambaye alikua anafanya njama za kuharibu ushahidi kwa mtuhumiwa aliyempa mimba mmoja wa wanafunzi katika shule hiyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles