25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wakulima wa Pamba Simiyu walilia bei elekezi

Samwel mwanga – Simiyu

Wakulima wa zao la pamba Mkoani Simiyu wamemwomba Rais John Magufuli kuingilia kati na kuitaka serikali kuangalia upya bei elekezi ya kununulia zao hilo kwa msimu huu kwani haimnufaishi mkulima isipokuwa kuwakatisha tamaa ya kuendelea kulilima.

Hivi karibuni serikali ilitangaza bei elekezi ni Sh 1200 kwa kilo moja ya ununuzi wa zao hilo sokoni katika musimu huu uliozinduliwa katika wilaya Tanganyika mkoani Katavi ikiwa na ongezeko la Sh 100 kulinganisha na musimu uliopita.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati na maeneo tofauti walimwomba Rais Magufuli kuwasaidia ili nao waweze kunufaika na zao hilo kama vile alivyowasaidia wakulima za zao la korosho.

“Kwa musimu huu wa kilimo tumejitahidi kulima zao la pamba kwa wingi kwa kufuata kanuni bora tulizoelekezwa na maafisa ugani ili tuweze kuongeza uzalishaji kwa ekari moja maana tulikuwa tunapata Kg 300 lakini kwa kilimo hiki tunategemea kupata kg 800 mara baada ya mavuno lakini kwa bei hii iliyotangazwa ya Sh 1200 kwa kilo bado ni vizuri Rais Magufuli aingilie kati walau bei iongezeke hadi kufikia  Sh 2500 kwa kilo,”amesema Joel John mkulima wa kijiji cha Sangaitinje wilayani Meatu.

Aidha wamesema kuwa  pamoja na serikali kuondoa changamoto ya soko huria lililokuwa likisababisha bei kushuka na kupanda mara kwa mara kwa kufufua vyama vya msingi vya ushirika na kuweka bei elekezi bado bei hiyo haimkwamui mkulima kutokana na gharama kubwa anazotumia katika uzalishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles