27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wavuvi wakabiliwa na tozo 10

ARODIA PETER – DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya kilimo, Mifugo na Maji imehoji wingi wa tozo, ushuru mkubwa unaotozwa kwa wavuvi nchini.

Akiwasilisha taarifa ya maoni ya Kamati hiyo bungeni leo, Mei 21, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa amesema kuna tozo nyingi na ushuru mkubwa wanaotozwa wavuvi hivyo kuathiri tija na ukuaji wa sekta hiyo.

Amesema kamati imebaini kuwa changamoto kwenye sekta ya uvuvi zimegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni wavuvi, wafanyabiashara na mawakala pamoja na wenye viwanda vya kuchakata samaki

“Kuna tozo nyingi, ushuru mkubwa wanaotozwa wavuvi ambao unajumuisha ushuru wa maegesho ya chombo.

“Tozo nyingine ni usajili wa mitumbwi, leseni ya uvuvi, leseni ya wavuvi, leseni ya Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na Nchi kavu (Sumatra).

“Pia kuna kodi ya mapato, vibali vya BMU, leseni za zimamoto, ushuru wa mazao ya samaki na leseni ya uvuvi katika kila halmashauri ambayo mvuvi ataenda kuvua”amesema Mgimwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles