Florence Sanawa, LindiÂ
Jeshi la Magereza mkoani Lindi limewashauri wakulima wa mbogamboga nchini kufuga sungura ili kuwapunguzia gharama za ununuaji wa dawa za kupulizia mboga na kuzuia kupatwa na magonjwa kwakutumia mkojo wa mnyama huyo.
Akizungumza na Mtanzania Digital Katika maonyesho ya nanenane kanda ya kusini Dk. Yusuph Seleman amesema kuwa endapo wakulima watafuga sungura kwa wingi wanaweza kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
“Unajua huo mkojo ni dawa nzuri ya kuzuia wadudu kushambulia mboga zikiwa shambani na unapotaka kutumia unalazimika kuweza maji kidogo” amesema Yusuph.
Naye Dk. Rashid Myao amesema kuwa sungura hao wanapatikana gereza Kingurungundwa lililopo mkoani humo ambapo wamekuwa wakilima mboga za aina mbalimbali na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa wamekuwa wakitumia kinyesi cha sungura Kama mbolea na mkojo kwa kuzuia wadudu.