Dstv yajikita kumuenzi King Majuto

0
1208

Amina Omari,Tanga

Kampuni ya ving’amuzi ya DSTV, imesema itajikita katika kuenzi kazi za marehemu Amir Athumani ‘king Majuto’ ili kuhakikisha vizazi vinavyokuja vinajua kazi zake.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja mauzo wa anda ya Kaskazini, Jackson Mark, wakati wa kumbukumbu ya kuenzi kifo cha msanii huyo ‘Majuto Day’. 

Naye Msemaji wa familia Mohamed Majuto, amesema kuwa ili kumuenzi marehemu tayari wako mbioni kuachia kazi ambazo alizifanya kabla ya umauti kumfika.

Naye msanii Rehema Abdallah amesema tayari wameshapata mbadala wa King Majuto ambaye anatarajiwa kutambulishwa nchini Kenya hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here