25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi wa Mwanza waombwa kujitokeza katika tamasha la kibiashara

Na Sheila Katikula,Mwanza

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la kibiashara (Tanzania Bussiness Summit) la utalii na uwekezaji linalotarajia kufanyika Aprili 30 hadi mei 2 jijini hapa mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa tamasha hilo, Bernad Mwata alimaarufu kama (Benking) amesema maonesho hayo yatafanyika Rock City Mall kwa siku tatu na yatahudhuliwa na viongozi mbalimbali na yatahusisha wafanyabiadhara kutoka nchini  Kenya, Burudi, Uganda, Rwanda na Afrika ya Kusini.

“Zaidi ya wafanyabiashara 1,000 wa sekta ya ukitalii kutoka nchini na nje ya nchi wanatarajia kukutana jijini hapa kwenye tamasha hilo lenye lengo la kuwaunganisha wafanyabiashara ili waweze kubadilishana mawazo na kufanyabiashara, kupata wateja wapya sanjari  kutangaza biashara na utalii kwa ajili ya kuwainua wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi,”amesema Mwata (Benking)

Amesema baadhi ya washiriki ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT),  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Idara ya Utalii, Hospitali ya Bugando, Bugando College of Health, TTCL, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Wengine ni Chloride Exide Tanzania, Niita Microfinance, benki ya  NMB, Tata, BMG, MCL, Tatol, Toyota, Nabaki Afrika, City aim, Vodaco, Tigo na Movit.

Akizungumza kwa niaba ya waandaaji wa jukwaa hilo, Mwenyekiti wa Kampuni ya Africity Mining, Charles Masanga amesema jukwaa hilo litaunganisha wafanyabiashara, kupeana mawazo na kuboresha kazi zao ili kuzidi kukuza uchumi wa Tanzania.

Ofisa Masoko wa TTB, Rhoda Kasame amesema wameandaa mpango wa wananchi na washiriki kuweza kutembelea vivutio vinavyopatikana mkoani Mwanza na nje ya Mkoa huo  kikiwemo kisiwa cha Saanane, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  na Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora.

Amewataka wakazi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi ili kujua mambo mbalimbali yanayohusu utalii na vivituo vilivyopo katika maeneo yao.

“Tutatoa taarifa kwa wale watakaoweza kupata fursa ya kutembelea hifadhi zetu za Taifa 22 ambazo zimetawanyika karibu Mikoa yote ya Tanzania ; hifadhi za Taifa zina vivutio vya kutosha kwa ajili ya watanzania tutumie fursa ya jukwaa hili kuja kujionea vivutio vyetu,”amesema Acceva Malya, Mkuu wa Hifadhi ya kisiwa cha Saa nane.Mwishoooo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles