25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

NazB Music aanika historia yake kimuziki

Zurich, Uswizi

Rapa kutoka Zurich, Uswizi, NazB Music, ameanika asili ya jina lake na jinsi familia na majirani walivyochangia kukuza uwezo wake kimuziki.

Akizungumzia hali hiyo, NazB Music mwenye asili ya Nigeria, amesema tangu utotoni alizungukwa na watu wanaotumia vyombo vya muziki kiasi kwamba akajikuta anapenda sanaa hiyo.

“Uvumilivu wangu mwishowe nilipewa jina la utani la Nazodobas ambalo mwishowe lilibadilika kuwa NazB na likawa jina langu kwenye muziki,” amesema NazB ambaye hapo kabla aliwahi kuishi kwenye nchi kama Mali, Ivory Coast, Ghana, Senegal, Afrika Kusini, Surinam na Brazil.

Katika kuendelea kuwapa burudani mashabiki zake, NazB Music ameachia wimbo, Wombolo aliomshirikisha Lekko.

“Mashabiki wanaweza kuingia kwenye tovuti yangu ya NazB.com ambapo hapo kuna muziki wangu wote hasa video ya Wombolo ambayo pia ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” amesema NazB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles