Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Wakazi wa Ukonga, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wametakiwa kupeleka watoto wao shuleni Gisela kwa elimu bora.Mkuu wa Shule ya Msingi Gisela ambayo ni ya Mchepuo wa Kiingereza, Malimi Kwilasa anasema kuwa shule hiyo imekuwa ikifaulisha kila mwaka kwa wastani mzuri wa daraja A na hivyo kuifanya kuwa moja ya shule bora Wilaya ya Ilala.
Pia shule hiyo ina shule ya awali au chekechea. Anasema matokeo ya mwaka jana darasa la saba shule ilikuwa na watahiniwa 92 kati yao waliofaulu kwa daraja la A ni 85 wakati daraja B ni saba tu.“Hivyo kwa mantiki hiyo utaona namna shule yetu inayofaulisha, wazazi wawalete watoto wao shuleni hapa,”anasema.
Anasema wakazi wa tarafa ya Ukonga kata ya Kipunguni wana fursa ya kupeleka watoto shuleni hapo ili wapate elimu bora, shule iko Mtaa wa Amani, barabara ya Bombambili.Mwalimu Kwilasa anasema kuwa mazingira ya kufundishia ni bora na shule ina usafiri kwa wanafunzi wa maeneo mbalimbali ya Ukonga na hata nje ya Ukonga.