25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wakandarasi waaswa kutekeleza miradi ya maji kwa wakati

Samwel Mwanga – Meatu

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Mzee Mkongea amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji nchini kuikamilisha kwa wakati uliopangwa kwa lengo la kuwanufaisha wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 23, mara baada ya kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Itinje ulioko wilayani humo ambapo amesema kuwa miradi mingi ya maji huwa haikamiliki kwa wakati huku akitolea mfano wa mradi huo ambao ulianza kutekelezwa tangu juni 2014 lakini hadi sasa haujakamilika.

“Miradi mingi ya maji inayosimamiwa na serikali haikamiliki kwa wakati na wakati mwingine fedha zinazotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo hutumika hovyo, mfano ni huu mradi ambao tuliopo sasa ulianza mwaka 2014 na ulitakiwa ukamilike juni 2016 lakini hadi leo haujakamilika na moja ya sababu ni mkandarasi kutokuwa na watalaamu wa kutosha, mtatoaje zabuni kwa mtu asiye na wataalamu wa kutosha na haya ni matumizi mabaya ya fedha za serikali?” amesema.

Aidha amemtaka mkandarasi anayejenga mradi huo kupima vifaa vya ujenzi ambavyo ni nondo na zege katika kipindi cha majuma matatu na kisha apatiwe taarifa sehemu yoyote watakayokuwepo huku akiwataadharisha viongozi wa halmashauri kutoa zabuni kwa upendeleo.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo, Mhandisi wa maji wilayani humo, Sylvester Pauline alisema mradi huo umelenga kuhudumia wakazi wapatao 3,962 na utagharimu kiasi cha Sh Milioni 450.26 hadi kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles