Mbunge: Vivutio vya Utalii vitangazwe

Ramadhan Hassan

Mbunge wa Mufindi Kusini Cosato Chumi (CCM), ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuvitangaza vivutio vya Utalii kama ambavyo Msemaji wa Simba Haji Manara anavyoitangaza Simba.

Chumi ametoa kauli hiyo leo Mei 23 bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa  mwaka 2019-2020.

Chumi amesema Manara anahamasisha Simba inajaza uwanja sasa ni kwanini wizara isimtumie ili kuvitangaza vivutio vya utalii.

“Katika suala la michezo kuna msemaji anaitwa Manara pia kuna Thobias Kifaru wa Mtibwa Sugar wale wanazitangaza timu zao sasa  kwanini tusihamashe watu waende katika vivutio vyetu kama ambavyo wanahamasisha wale wasemaji.”amehoji Chumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here