24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wakala achangia Toure kusugua benchi

maxresdefault

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure, amekuwa akikaa benchi katika klabu hiyo kutokana na maneno ya wakala wake Dimitri Seluk, kwenda kwa kocha wa klabu hiyo, Pep Guardiola.

Inadaiwa kwamba, Toure alikuwa hana maelewano mazuri na kocha huyo tangu wakiwa katika klabu ya Barcelona mwaka 2008, hivyo kocha huyo alichukua hatua ya kumuuza Toure ndani ya Man City.

Kitendo hicho cha Guardiola kutofautiana na mchezaji huyo, wakala alimjia juu kocha huyo kwa kumshambulia maneno machafu ambayo yalimchukiza Guardiola.

Guardiola alipojiunga na Manchester City mwaka huu aliamua kukumbushia mgogoro wake na kiungo huyo kwa kumuweka benchi mara kwa mara katika michezo mbalimbali, huku mchezaji huyo akiwa na mchango mkubwa ndani ya mafanikio ya klabu hiyo tangu kujiunga kwake.

Kitendo cha Toure kukaa benchi kilikuwa na maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa soka, lakini kocha huyo akaweka wazi kuwa anatakiwa kuombwa radhi na mchezaji huyo pamoja na wakala wake.

Baada ya Toure kukaa benchi kwa muda mrefu na kuamini kuwa anapoteza kiwango chake anapokaa nje, akaamua kutumia ukurasa wake wa Facebook kumuomba radhi kocha huyo, lakini cha kushangaza ni kwamba wakala Seluk hataki kuomba radhi kwa kocha huyo huku mteja wake akiona kuwa anateseka benchi.

Kutokana na hali hiyo, Guardiola ameweka wazi kuwa alisaidia radhi ya Toure bila wakala wake kuomba na yeye, hivyo akishindwa kabisa kufanya hivyo basi maombi ya Toure hayana faida yoyote kwake.

Kwa mujibu wa mtandao wa talkSPORT, wakala huyo ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuomba radhi kwa kuwa hana kosa lolote alilolifanya kwa kocha huyo labda mchezaji mwenyewe.

“Sina mpango wa kuomba radhi. Tunataka amani lakini siwezi kuomba radhi. Niombe radhi kwa jambo lipi? Labda Toure anaweza akaomba radhi lakini kwa upande wangu sijui niombe radhi kwa jambo lipi, ninaamini hata Toure ameomba radhi kwa ajili ya kutaka amani yeye na kocha wake.

“Ninaamini mashabiki wengi wanataka kumuona Toure akiwa uwanjani na mchezaji mwenyewe anataka kuisaidia klabu yake kupata matokeo mazuri.

“Tunataka kuleta amani kati yangu, Guardiola na Toure kwa ajili ya mashabiki, pamoja na kupata matokeo mazuri uwanjani.

“Mchezaji kama Toure ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa pamoja na kulipwa fedha nyingi, hatakiwi kukaa nje ya uwanja bila kucheza kwa muda mrefu,” alisema Seluk.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles